Wakazi watanga kuchukua sheria mikononi dhidi ya wahalifu wanao kamatwa na kuachiwa bila kuchukuliwa hatua


Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, wilaya Arumeru na Diwani wa Kata ya Mlangarini, wilayani humo, Mathias Manga, amenusurika kufa, usiku wa kumakia leo, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kumuumiza maeneo ya mbavu za kulia.

Akizungumza leo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea Juni 23 mwaka huu, majira ya saa 4:45 eneo la Ngarenaro na majeruhi pia ni mfanyabiashara mkubwa wa madini ya Tanzanite.

Amesema Manga alikuwa akitoka katika shughuli zake za kawaida na alipokuwa anarejea nyumbani kwake eneo la Ngarenaro, kwenye nyumba za Shirika la Nyumna la Taifa, ghafla aliona gari likimfuata kwa nyuma na alipokuwa akitembea kwa kasi nalo liliongeza mwendo.

Sabas amesema Manga akahisi hao watu wanamfuata, hivyo akazidi kuongeza mwendo hadi alipofika getini kwake nalo lilipaki kwa nyuma yake na akashuka mtu mmoja, akiwa ameshika kisu na mara mwingine akiwa ameshika bunduki na ndipo alipolazimika naye kutoa silaha yake yake.


Amesema Manga alipotoa silaha yake ili kujiami, alishtukia amepigwa risasi na kwa bahati nzuri haikumpata vizuri, ilimpitia maeneo ya nyama kwenye mbavu upande wa kulia na watu hao waliondoka na walikuwa watano.
Wakazi watanga kuchukua sheria mikononi dhidi ya wahalifu wanao kamatwa na kuachiwa bila kuchukuliwa hatua Wakazi watanga kuchukua sheria mikononi dhidi ya wahalifu wanao kamatwa na kuachiwa bila kuchukuliwa hatua Reviewed by KUSAGANEWS on June 24, 2015 Rating: 5

No comments: