Liverpool yakataa tena kumuuza Sterling


 Klabu ya Liverpool imekataa rasmi ombi la pili la Manchester City la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling.

Inaaminika kuwa ombi hilo jipya lilikuwa la kitita cha pauni milioni 35.5 ambacho kingeongezwa na kufika pauni milioni 40.

Sterling mwenye umri wa miaka 20 ambaye amehusishwa na Arsenal pamoja na Real Madrid ana thamani ya pauni milioni 50 kulingana na Liverpool.

Wiki iliopita Liverpool ilikataa kitita cha pauni milioni 25 kutoka kwa Manchester City.

Sterling alijiunga na Liverpool kutoka QPR mwaka 2010 na sasa yuko katika kandarasi hadi mwaka 2017,lakini amekataa ombi la malipo ya kitita cha pauni 100,000 kwa wiki.
Liverpool yakataa tena kumuuza Sterling Liverpool yakataa tena kumuuza Sterling Reviewed by KUSAGANEWS on June 18, 2015 Rating: 5

No comments: