Mauaji yaliyoifanywa siku chache zilizopita na kundi la al Shabab dhidi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Garissa huko mashariki mwa Kenya yamezusha hasira kubwa ndani na nje ya nchi hiyo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kuna wasiwasi Wakenya wakatoa radiamali kali dhidi ya msimamo dhaifu wa serikali ya Kenya katika kukabiliana na mashambulizi ya kundi hilo la kigaidi. Ayo Johnson ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Afrika aliyeko London,
Uingereza ameambia IRIB kwamba shambulizi la Garissa si la kwanza kufanywa na kundi hilo dhidi ya Kenya na yumkini halitakuwa la mwisho. Ayo Johnson amesema, iwapo serikali ya Nairobi haitachukua hatua za maana na kubwa ipasavyo za kukabiliana na mashambulizi ya al Shabab, basi inapaswa kujitayarisha kwa wimbi kubwa la hasira za wananchi.
Baada ya mauaji ya kutisha ya watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa huko kaskazini mashariki mwa Kenya, jumuiya mbalimbali za kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na nchi nyingi duniani zimelaani mauaji hayo na kutilia mkazo udharura wa kukabiliana vilivyo na ugaidi.
Pamoja na hayo wachambuzi wa mambo wanakubaliana kwamba, wananchi wa Kenya ndio wanaoendelea kuwa wahanga wa ugaidi wa kundi la al Shabab. Kamanda wa kundi hilo amedai kuwa mauaji ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Garissa yamefanyika kulipiza kisasi cha kutumwa majeshi ya Kenya huko Somalia katika operesheni ya kikosi cha AMISOM. Kenya inashirikiana na nchi nyingine kadhaa katika kikosi hicho kwa ajili ya kuliangamiza kundi la al Shabab nchini Somalia.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment