Mchezaji gofu ya kulipwa nchini
Kenya ametimuliwa mashindanoni baada ya kufoka kwenye mtandao wake wa
Facebook kuwa alikuwa amebaguliwa kwa msingi ya rangi yake katika klabu
ya gofu ya Karen.
\
Hatua hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa
wapenzi wa gofu baada ya kudai kuwa alibaguliwa kwa misingi ya rangi
yake katika klabu ya gofu ya Karen.Kupitia mtandao wake wa Facebook Richard Ainley aliwaambia wafuasi wake kuwa alikuwa amebaguliwa alipokuwa akitaka kuegesha gari lake
kabla ya kushiriki mkondo wa kwanza wa mchuano wa Gofu ya kimataifa ya Kenya Open ulioanza mapema leo.
Mashindano hayo yanayoandaliwa kila mwaka ni sehemu ya ligi ya kimataifa ya gofu ya European tour.
Ainley alisema ''Looooo kumbe ukoloni bado upo Kenya !''
''Nimelazimika kutembea mwendo mrefu nikikokota gari langu la vigongo baad ya kunyimwa ruhusa ya kuegesha gari langu
ndani ya klabu ya gofu ya Karen licha ya kuwa mimi ni mkenya naambiwa kuwa ni Wazungu na waafrika wachahe tu wanaoruhusiwa kuingia humu''
hawajui kuwa mimi ni mchezaji wala hawataki kujua.
''Shindwe !Kwa hakika imenikera sana '' alifoka Ainley
Muda mchache baadaye Ainley aliitwa katika afisi za mwendesha mashindano wa klabu hiyo na kuelezwa kuwa alikuwa amekiuka sheria maadili na ustaraabu
wa klabu hiyo ya Karen na hivyo hatoruhusiwa kuendelea na mashindano.
''Nimekatazwa kuchezwa kwa sababu ukweli wa hali kama nilivyo andika awali katika mtandao wangu wa Facebook.
.
Mkenya atimuliwa kwa sababu ya rangi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2015
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment