Mancity yawalenga nyota 3 wa Liverpool

Mabingwa hao wanapanga kukibadilisha kikosi hicho hatua ambayo huenda ikawakosesha taji lolote.

Mwenyekiti Khaldoon Al- Mubarak ameandika majina ya baadhi ya wachezaji wakiwemo nyota wa England Raheem Sterling na Jordan Henderson.

Imebainika kuwa kilabu hiyo pia inapanga kumnunua mchezaji wa Brazil Coutinho.
Inadaiwa kuwa wakuu wa kilabu hiyo wanaamini Coutinho anaweza kuhamishwa hadi katika uwanja wa Etihad kwa kitita sha pauni millioni 20 iwapo Liverpool itashindwa kuorodheshwa miongoni mwa timu nne bora zitakazofuzu kucheza katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Habari hizo huenda zikamshtua Brendan Rodgers ambaye anawaona wachezaji wake wakiwindwa na kilabu pinzani.

Rodgers angependa sana kuwazuia wachezaji wake katika uwanja wa Anfield lakini pia anajua kwamba hawezi kushindana na mfuku mzito wa mmiliki wa kilabu hiyo Sheikh Mansou
Mancity yawalenga nyota 3 wa Liverpool Mancity yawalenga nyota 3 wa Liverpool Reviewed by KUSAGANEWS on April 09, 2015 Rating: 5

No comments: