Yanga inaongoza ligi kuu bara ikiwa na pointi 46, inafuatiwa na Azam FC yenye pointi 38 na Simba iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35
KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm, amejigamba kikosi chake ni kipana na kinaweza kupambana kwenye mazingira tofauti iwe kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara au ile ya Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki hivisasa.
Pluijm ameiambia Goal kikosi chake kwa sasa kiko katika ubora wake kutokana na ufiti waliokuwa nao wachezaji wake ambao pia wanapenda kupata mafanikio.
“Nina orodha kubwa ya wachezaji wenye uwezo na vipaji vya juu kwa hiyo ndiyo maana hukuona pengo la Andrey Coutinho tulipomkosa kwa mwezi mmoja na hata sasa tunaelekea kucheza na Etoile Sportive du Sahel tunaweza kumkosa Salum Telela inauma lakini tunaye mtu wakuziba nafasi yake,”amesema Pluijm.
Yanga inaongoza ligi kuu bara ikiwa na pointi 46, inafuatiwa na Azam FC yenye pointi 38 na Simba iko nafasi ya tatu
Hans van der Pluijm: “Nina wachezaji wenye uwezo na vipaji vya hali ya juu”
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 18, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment