Serikali
ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya
kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo.
Serikali imewapa wale wote waliopokea mafunzo kutoka kwa Al Shabaab siku kumi kupiga ripoti kwa afisi za wasimamizi wa miji ya Garissa, Mombasa ama Nairobi.
Waziri huyo wa usalama pia amechapisha nambari za simu ambazo vijana hao wanaweza kutumia kutoa ripoti hizo kisiri.
Amesema wale watakaoitikia mwito wake watasamehewa na kupata usaidizi wa kurejea katika jamii.
Hata hivyo amewaonya wale ambao hawatafanya hivyo katika siku kumi zijazo kwamba serikali itakabiliana nao kama wahalifu kwa mujibu wa sheria za Kenya.
Wazazi ambao wanao wametoweka, au wanaojua kuwa wamejiunga na Al Shabaab ama kuuwawa nchini Somalia wametakiwa kutoa ripoti hizo kwa serikali la sivyo wafunguliwe mashtaka kama washiriki wa magaidi.
Hofu imeibuka nchini Kenya baada ya ripoti kwamba mmoja wa wanamgambo walioshambulia chuo kikuu cha Garissa na kuchangia kuwaua watu 147 alikuwa Mkenya aliyesomea taaluma ya sheria jijini Nairobi.
Babake, ambaye ni chifu, alipiga ripoti kwa serikali alipotoweka mwanawe miaka miwili iliyopita.
Al Shabaab:Msamaha wa siku 10 Kenya.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment