Waziri Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa jana Jumanne Septemba 24,2024 ameungana na wakuu wa nchi na Serikali katika ufunguzi wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja na Mataifa (UNGA79)uliofanyika makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani .
Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Gutteres ambapo Waziri Mkuu anashiriki kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan .
Majaliwa anatarajiwa kutoa tamko la Serikali kwenye mkutano huo Ijumaa Septemba 27,2024 akiwa ni Waziri Mkuu wa Pili kuhutubia baraza hilo.
MAJALIWA ASHIRIKI UFUNGUZI UNGA79 KUHUTUBIA SEPTEMBA 27.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 25, 2024
Rating:
No comments:
Post a Comment