Matapeli
waliotambulika kwa majina ya Innocent Joseph na Kakamba, Iden na Wenzao
wawili, wanaotokea Kampuni ya Utafiti ya Research Solution Africa,
wamekuwa wakifanya kazi ya kupokea Tenda za Research na watu wamekuwa
wakilipwa kwa siku, usiku na mchana ikitegemea na mteja anayefadhili
zoezi hilo la utafii.
Mfano
miongon mwa benki zinazodhamini ni World Bank ambapo huwa wanawalipa
watu kiasi cha Sh. 25,000/= kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na iwapo
watasafiri mikoani vijini watalipwa kiasi cha Sh. 65,000/=.
Watajwa,
hapo juu hivi sasa wanatafutwa kutoka na matukio kadhaa ya kitapeli
waliokwisha yafanya siku za hivi karibuni ambapo mwezi uliopita
walitangaza tenda ya ‘Research Vacancy’ na kukusanya wanafunzi wengi tu
na wafanyakazi kadhaa waliofika kujiandikisha ili kushiriki mafunzo hayo
kwa ajili ya kupewa safari hizo za kwenda kufanya utafiti mikoani.
Watu
hao baada ya kujiandikisha walifanyiwa enterview na kama watu 100, hivi
wakaambiwa wamechelewa nafasi zimejaa, hivyo wakajengewa mazingira ya
utaratibu wa kutoa kitu kidogo, yaani pesa ili kuwawezesha kupata
research kwa muda wa miezi mitatu na kupangiwa kulipa kiasi cha Sh. 300,
000/= kwa kila mmoja wao kwa watu 130.
Watu
walianza mafunzo na wakaanza kulipwa kiasi cha Sh. 10,000 na kuahidiwa
kwenda field kwa muda wa wiki moja baada ya mafunzo hayo.
Baada
ya mafunzo watu walipangiwa kwenda kufanya Field katika Mkoa wa Dar es
Salaam, Pwani, Bagamoyo, Kibaha na Kijichi for Pilots na wakati
wakipangiwa kuondoka juzi kuelekea kuanza field kwamalipo ya Sh.90,000/=
kwa siku ambapo malipo yangefanyika kila baada ya siku 10, ambapo
kilamwanafunzi baada ya kupiga hesabu aliona kuwa inawalipa kiasi cha
kutoona hasara kulipia kiasi cha sh 300,000, 400,000 na 500,000 kwa kila
kichwa kulingana na field hitajika.
Watu
hao walikuwa wakiendesha mafunzo hayo katika Kumbi za hoteli kubwa
kubwa kama Ubungo Plaza,Magomeni na nyinginezo, ambapo watu hawatayari
wamekuwa na kundi kubwa lililosambaa hadi mikoani na mafunzo ya mwisho
hivi majuzi walifanyia katika ukumbi wa Nguruko uliopo Mbezi Beach,
Interchick.
Na
katika baadhi ya mikoa kama Morogoro, Arusha na kila Mkutano mmoja wa
mafunzo hayo ulikuwa na takriban watu 100 hadi 130, jambo lililowafanya
kukusanya jumla ya kiasi cha Sh. milioni 100 hadi 130.
Ilikuwa
ni siku ya Ijumaa mida ya saa mbili usiku maeneo ya Mbezi Juu kwa
Sanya, kulizuka kundi la viana kama 20, waliovamia nyumba ya mmoja wa
matapeli hao na kumkuta mkewe na kumuweka chini ya ulinzi ili apatikane
mumewe huyo, aliyetambulika kwa Jina la Innocent Joseph.
Vijana
hao baada ya kujieleza kwa wakazi wa eneo hilo baada ya kushukiwa kuwa
ni wahalifu, walifafanua na kuelezea mchakato mzima tangua
wanachangishwa fedha na kuhudhuria mafunzo hadi siku waliyokimbiwa na
kuulizia makazi yake hadi walipofikishwa nyumbani kwake anapopanga.
Baada
ya watu hao kufika eneo hilo na kuonyeshwa nyumba anayoishi watu hao
walionyesha mshangao mkubwa baada ya kuona nyumba hiyo ambapo wao
walihisi kukuta bonge la nyumba na bila kujua kua hata nyumba hiyo pia
alikuwa amepanga.
Watu
hao walimkuta mkewe na kukaa ndani hapo hadi usiku majira ya saa tano
hadi walipofika wakati wa eneo hilo na Mjumbe wa eneo hilo na kuzungumza
nao na kugundua kuwa hawakuwa wahalifu bali walikuwa wakidai haki zao
na kuomba mikeka ili kukesha nje ya nyumba hiyo kumsubiri mtuhumiwa wao.
watu
hao walikesha hadi asubuhi bila mafanikio kwani asubuhi yake walikuwa
hata ile familia ya mtuhumiwa wao waliyoikuta usiku tayari ilishatoroka
bila kujua ilikopiyia na simu ya mtuhumiwa wao haikupatikana tena na
kuamua kuondoka.
Siku
ya pili walikuwawatu wengine zaidi ya waliokuja jana yake na kutafuta
hadi kupata nyumba ya mtuhumiwa wao na kukuta imefungwa na baadhi yao
kuamua kwenda kubomoa mlango na kujisevia baadhi ya vitu kama Flat
Screen, Viatu,Sab oofa, Redio na vinginevyo na kusepa navyo.
Namba za matapeli hao ni Aiden 0652213731 na Innocent 0715075807
Shime Watanzania tukomeshe utapeli huu, mtumie kila rafiki yako ili wakamatwe watu hawachanzo full shangwe blog
VIJANA HAWA WALIMU WANATAFUTWA NA WANAFUNZI WAO BAADA YA KUINGIA MITINI NA PESA ZA FIELD
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment