Wakati ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume
huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za
kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako
mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.
Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17,
wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi,
iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka
25.
Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa,
limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.
Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa
kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na
uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.
Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na
mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa
kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi
karibuni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya
mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni
hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya
ualimu chuoni.
“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina
uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na
uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni
sawa tu", alisema Mwalimu mkuu.
“Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba
ya ualimu. Hii kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira
yake ya kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu
masomo yake…” alisema. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa
tayari ni mtu mzima.
“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji
… Mwalimu mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa
amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.”
Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi
wake hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia
ujauzito mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.
Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo
zimegonga mwamba baada ya watu wao wa karibu kulieleza gazeti hili kuwa hawako
tayari kuuzungumzia mkasa huo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa
habari hizi kwa masharti ya kutoandikwa gazetini kwa hofu ya kuchukuliwa hatua
za kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya
mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo
amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao.
Walisema pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao
ameathirika kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye
kwa sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.
“Huyu mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu
alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa
ameweza kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi
limehamia kwa mwalimu mwenzake,“ alisema mmoja wao.
Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa
mwanafunzi huyo hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake
huyo, hivyo hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na
jinsi, bali kukubaliana na matokeo.
“Usiniandike jina gazetini, sisi tunashauri mwalimu huyo
wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe
shule nyingine kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa
na watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.
“Isitoshe tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama
angekuwa ni mwalimu wa kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito
angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo
kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?” Alihoji.
Baadhi ya wazazi mkoani hapa waliohojiwa na mwandishi wa gazeti
hili kwa nyakati tofauti wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa
jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi
MWANAFUNZI AMTIA MIMBA MWALIMU WAKE ANAYEMFUNDISHA DARASANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment