Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
leo Machi 12, 2018 imezifuta kesi mbili za makosa ya mtandaoni, namba 325/17 na
333/17 zilizokuwa zikiwakabili Obadiah Frank Kiko Mkazi wa Chato mkoani Geita
na Hafidhi Khamis kutoka Zanzibar baada ya upande wa Jamhuri kushindwa
kukamilisha ushahidi.
Uamuzi huo umekuja baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya
Kisutu, Wilbard Mashauri kutoa angalizo kwa upande wa jamhuri kufuatia
kushindwa kuwasilisha ushahidi wao kwa zaidi ya mara tatu mahakani hapo.
Wakili upande wa utetezi, Wakili Msomi Alex Massaba amesema
baada ya watuhumiwa hao kuachiwa huru na mahakama, walikamatwa tena na
kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Amesema wanapanga kwenda Mahakama Kuu kuomba tafsiri ya kifungu
namba 225 (5) cha Sheraia ya Makosa ya Mtandaoni kwa madai kuwa kinatumiwa
vibaya na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WATUHUMIWA MAKOSA YA MTANDAONI, POLISI YAWADAKA TENA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment