Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) Mohammed Mchengerwa amesema Serikali itapeleka Sh 3.2 bilioni Peramiho ,mkoani Ruvuma kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha afya ,shule ya Serikali na barabara ya lami.
Mchengerwa ameyasema hayo jana Jumanne Septemba 24,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Peramiho kwenye Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan .
Aidha amesema Rais ameelekezwa sh600 million zipelekwe kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari katika jimbo hilo.
Leo Jumatano ,Rais Samia anaingia siku ya Tatu ya Ziara yake ya Kikaz mkoani Ruvuma inayotarajiwa kuhitimishwa Septemba 28,2024 kwa mkutano na hadhara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji .
SH3.2 BILIONI KUTUMIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU AFYA ,ELIMU NA BARABARA PERAMIHO .
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 25, 2024
Rating:
No comments:
Post a Comment