Waziri mpya wa Afya ,Jenista Mhagama amezitaka Hospitali zote na vituo vya Afya Nchini kuhudumia Wagonjwa wa nje wanaofika kupata huduma kwa saa zisizozidi tatu .
Waziri ameserma hayo leo August 20,2024 wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General ) ili kuona hali ya utoaji wa huduma sambamba na kuongea na watumishi waliopo Hospitaini hapo .
Amezitaka Hospitali zote Nchini na kuziagiza kuzingatia mzunguko wa utoaji wa huduma kwa Wagonjwa na kuhakikisha mzunguko huo unatumia saa za kitaalamu ambayo hazizidi tatu kwa kila Mgonjwa na kupunguza muda wa wagonjwa kukaa hospitalini kusubiri huduma .
ili kufanikisha hilo Waziri Mhagama amesisitiza uwepo wa matumizi ya TEHAMA pamoja na mifumo ya kusomana ikiwa ndiyo njia pekee ya kuokoa muda na kutoa huduma bora kwa Mgonjwa ikiwa ni sehemu ya kupunguza malalamiko ya mara kwa mara.
WAZIRI WA AFYA ATOA TAMKO MGONJWA AHUDUMIWE SAA ZISIZOZIDI TATU.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2024
Rating:
No comments:
Post a Comment