Wananchi wanaoishi katika mikoa ya Dar es salaam ,Tanga ,Pwani ,Lindi ,Mtwara ,Pemba na Unguja wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano mfululizo .
Taarifa hii ya uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku hizo tano imetolewa jana Jumanne Agosti 20,2024 na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Athari zinazotarajiwa kutokana na hali hiyo mbaya ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi ,uvuvi ,na usafirishaji wa watu na vitu baharini .
Pia leo Jumatano Agosti 21 ,2024 TMA imetoa angalizo la upepo mkali wa kilomita 40kwa sasa na mawimbi makubwa yanayofika mita mblii.
TMA YATOA TAHADHARI KUTOKANA NA UWEPO WA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO NDANI YA SIKU SABA .
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2024
Rating:
No comments:
Post a Comment