Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) kimetaka Tume ya Mipango kuongeza wigo wa utawala bora katika Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 na kuwapa nafasi ya kutosha wananchi kuchagua viongozi wanaowataka .
Hayo yameeleza hii leo Jumatano Agosti 21,2024 Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar ),Salum Mwalim katika mkutano wa kukusanya maoni kuelekea maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo 2025-2050 kwa viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Tume ya kukusanya Maoni kuhusu dira hiyo ,iliyokutana na vyama vya siasa jijini hapa,akisema utawala bora utafanikisha mipango ya maendeleo kwa kuwashirikisha wananchi.
Mwalimu amesisitiza kuwa utekelezaji wa dira hiyo unategemea sana utawala bora na viongozi wenye uelewa ,wivu wa maendeleo na utayari wa kusimamia na kutekeleza dira hiyo.
Katika maoni yake , Mwalimu pia ameeleza kuelekea miaka 25 ijayo ,msingi mmoja wapo wa utaifa uwe ni wakuheshimiana miongoni mwa Watanzania ,huku msisitizo ukiwekwa kwenye uvumbuzi na ubunifu ,pamoja na kukuza siasa safi ili nchi iweze kusonga mbele na kwenda sambamba na mataifa mengine duniani.
No comments:
Post a Comment