Raisi wa Tanzania Dkt . Samia Suluhu Hassan leo August 20,2024 amezindua Shule ya Maandalizi iliyojengwa na benki ya NMB katika eneo la Tasani Makunduchi Mkoa wa kusini Unguja Visiwani Zanzibar na kupewa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan .
Akiongea baada ya uzinduzi huo Raisi Samia amesema 'Sasa nitoe shukrani kubwa sana kwa NMB Bank kwa kufadhili ujenzi wa shule hii lakini kama alivyosea Mtendaji Mkuu Bi Ruth .kwamba toka tumeanza hili Tamasha ,NMB wamejitoa sana sio shule hii tu kuna maeneo mengine wamejenga miradi inayofanana na hii ,tunashukuru sanasana na tunategemea uwepo wanu na kazi yenu'
'Hii ni Shule ya mfano pengine ndani ya Wilaya nzima niombe huu sasa uwe ndio mfano wa Shule zetu za makuzi ya awali ya Watoto wetu ,mkiongeza ukubwa sio neno lakini ubora na huduma zilizopo ,ukiangalia shule hii hakuna kisichokuwepo ,maji tanki lipo ,umeme wa kutosha ,NMB imeeka hadi ACCOUNT ,Hapa kilichobaki Wazazi mkileta Watoto muweke na pampers kwenye mabegi ili watoto wabadilishwe na wakue vizuri akisema Raisi samia
No comments:
Post a Comment