Waziri Mkuu Kassim Majaiwa ameshtushwa na madai ya madereva wa Serikali kulogana ili wapate magari ya kufanyia kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaoendelea jijini Arusha kwa siku nne mfuluizo
Mtanda amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakilogana ii wapate magari ya kuendesha kutokana na vyombo vyao kuharibika na kuishia kukaa kwenye ajira wakilipwa mishahara bila kupangiwa majukumu ,hivyo baadhi hufanya mambo hayo wapangiwe kazi.
Akizungumza leo Agosti 20,2024 ,Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu wote wa taasisi wa hakikishe wanafanya tathimini ya magari yote ya Serikali yaliyoharibika yatengenezwe ,na kuhakikisha madereva wote walioajiriwa wanapata vyombo vya kufanyia kazi.
Hivyo sasa nitumie nafasi hii,kuwaagiza wakuu wote wa taasisi na waajiri waanze kufanya tathmini mapema sana ya kufufua magari ya serikali yaliyoharibika ili madereva wapangiwe kazi wasilogane kugombea machache yaliyopo 'amesema.
Mbali na hilo ,amewataka waajiri kubainisha madereva waliopo kweny taasisi zao ambao hawana vyombo vya kufanyia kazi au hawajapangiwa majukumu ,ili serikali iwatambue na kuwapangia kazi.
No comments:
Post a Comment