CHAMA CHA WANASHERIA ;HUDUMA ZA KIJAMII ZIWEPO NGORONGORO.











 Chama cha Wanasheria TLS kimesema baada ya kuona video katika mitandao ya kijamii zikionesha maandamano yaliyofanywa August 18 ,2024 na Mamia ya Wananchi wa Ngorongoro wakidai kuheshimiwa kwa haki zao ,na serikali kurudisha huduma zote za kijamii kwa wananchi wa Ngorongoro kwa kuwa ni haki zao ,pia vituo vya kujiandikisha kwa ajili ya kupigia kura ambavyo Wananchi wa Ngorongoro wanalalamika kwamba havipo katika maeneo yao virudishwe . 


Akiongea Jijini Dar es salam leo August 20,2024 Raisi wa TLS ,Boniface Mwabukusi amenukuiwa akisema yafuatayo Katika maandamano yao miongoni mwa mambo mengine ,Wananchi hao wamesikika wakilalamika kuondolewa kwenye maeneo yao kinyume na utaratibu bila wao kuridhia pamoja na kuondolewa kwa huduma zote za kijamii kama vile Shule ,huduma za afya pamoja na Maji ,kutokuwepo kwa huduma hizi muhimu kumepelekea Wananchi hao kuendelea kuishi katika mazingira magumu'


'Tamko la  Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Watu wa Asili la Mwaka 2007 limeeeleza wazi katika idara ya 10 kwamba watu wa asili hawatoondolewa kwa nguvu kutoka kwenye ardhi au maeneo yao , uhamisho wowote wa watu wa asili hauwezi kufanyika bila idhini yao huru kwa mujibu wa idara ya 24 ya katibu ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania ya mwaka 1977,kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo .


'Haki  ya kumiliki mali ni moja ya haki ya msingi ya binadamu .idara 24 imeeleza wazi kwamba Mtu yeyote hatonyang'anywa  Mali yake isipokuwa kwa taaratibu za kisheria ikiwepo ulipwaji wa fidia stahili'


'TLS  inatoa rai kwa Serikali kuonesha nia yake ya dhati kwa kurudisha huduma zote za kijamii  kwa Wananchi wa  Ngorongoro kwa kuwa ni haki yao  ,pia vituo vya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura  ambavyo Wananchi wa Ngorongoro wanalalamika kwamba havipo katika maeneo yao virudishwe ili wapate kutumia haki zao kwa kikatiba ya kujindikisha na kuboresha taarifa zao kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwezi wa November mwaka 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2025    Raisi wa TLS Boniface Mwabukusi.

CHAMA CHA WANASHERIA ;HUDUMA ZA KIJAMII ZIWEPO NGORONGORO. CHAMA CHA WANASHERIA ;HUDUMA ZA KIJAMII ZIWEPO NGORONGORO. Reviewed by KUSAGANEWS on August 20, 2024 Rating: 5

No comments: