Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelaani kitendo cha kukamatwa na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa Chama hicho Wilaya ya Temeke na kusema kukamatwa kwao ni kinyume cha sheria .
Taarifa ya CHADEMA iliyotolewa na mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje John Mrema ,imesema viongozi wawili wa wilaya ya Temeke waliokamatwa ni Jacob Mlay ambae ni katibu wa jimbo la Temeke ,Deusdedith Soka ambae ni mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Temeke huku mwingine aliyekamatwa akitajwa kuwa ni Dereva wa bodaboda Frank Mbisa .
Namba ya simu ya Deusdedith Soka ambayo inashikiliwa na Polisi tangu September 2023 imetumika kutuma ujumbe wa simu kwa Mwenyekiti wa Chama Wilaya ya Temeke wenye maudhui kuwa Deusdedith Soka kwenda Nje ya Nchi sababu ndani ya Chama kuna Migogoro hivyo anaondoka hadi baada ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa itakapokamilika na kusitisha maandamano ya tarehe 26 Agosti 2024,imeeleza taarifa ya CHADEMA
'Tunalitaka JeshI la Polisi liwaachie mara moja bila masharti na kama wametenda kosa lolote wafikishwe Mahakamani mara moja,Aidha Polisi ieleze inakowashikilia ii waweze kupata msaada wa kisheria na mahitaji muhimu ya kibinadamu 'imeeleza taarifa ya CHADEMA .
No comments:
Post a Comment