Klabu ya KMC FC inakabiliwa na changamoto ya
wachezaji sita tegemeo ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho
ambapo kwasasa wanaendelea na matibabu.
Wachezaji hao ni Hance Masound ambaye aliumia
jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Singida Big
stars na hivyo kushindwa kuendelea jambo lililopelekea kukimbizwa Hospitali na
gari la wagonjwa (Amblece).
Wachezaji wangine ambao jana walishindwa
kuendelea na mchezo mbali na Hance Masound ni Ibrahim Ame, Baraka Majogoro
ambao pia kwa nyakati tofauti katika mchezo huo uliomalizika kwa KMC FC
kupoteza kwa bao moja ugenini walishindwa kuendelea na mchezo kutokana na
kupata majeraha.
Aidha wachezaji wengine ni Kelvin Kijili,
Awesu Ally Awesu pamoja na Emmanuel Mvuyekure ambao hawa pia walikuwa na
majeraha ya muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kusafiri na Timu kwenye
mchezo dhidi ya Singida big Stars.
"Kwasasa tunakabiliwa na changamoto kubwa
ya wachezaji wenye majeraha, na ukiangalia kwenye Timu kila mchezaji anamchango
mkubwa pindi anapopewa majukumu na kocha, hivyo nikipindi kigumu lakini
tutajitahidi kadiri tuwesavyo ili kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja.
Katika hatua nyingine KMC FC imerejea Jijini
Dar es salaam alfajiri ya leo ikitokea mkoani Singida na kwamba kesho itaanza
kufanya maandalizi kuelekea katika mchezo unaokuja dhidi ya Tanzania
Prisons utakaopigwa Novemba 28 katika uwanja wa Uhuru Jijini hapa.
Imetolewa leo Novemba 24
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC.
No comments:
Post a Comment