Vicheko
vitaendelea kutawala Oktoba kwa watumiaji wa mafuta kufuatia kushuka kwa bidhaa
za mafuta kama mwenendo wa bei ulivyotolewa leo Oktoba 4.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)
inaonyesha kuwa bei za mafuta kuanzia Oktoba 5 zimeshuka hivyo petroli katika
jiji la Dar es Salaam itauzwa Sh2,886 kwa lita, dizeli Sh3083 na
mafuta ya taa Sh3,275 kwa lita.
Kulingana na taarifa hiyo kushuka kwa bei za mafuta kumetokana na
kushuka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia kwa Agosti 2022, ambazo
zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini katika mwezi wa Oktoba
2022 zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 na 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na
mafuta ya taa, mtawalia, ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Julai 2022.
“Hata hivyo, ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika
katika kukokotoa bei za Septemba 2022, gharama za uagizaji wa mafuta
zimeongezeka kwa kati ya asilimia 50 na 163 kwa kutegemea bandari na bidhaa
husika ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika katika kukokotoa bei
za Septemba 2022, na hivyo kuathiri mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini.
“Pamoja na hayo, kufuatia dhamira ya Serikali ya kuendelea
kupunguza madhara ya ongezeko la bei za mafuta hapa nchini kwa wananchi na
uchumi kwa ujumla, Serikali imetoa ruzuku ya Sh59.58 bilioni kwa ajili ya bei
za mafuta ya Oktoba 2022,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na
Mkurugenzi wa Ewura Modestus Lumato.
No comments:
Post a Comment