Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Monica Ndyekobora wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au laa.
Zumaridi
na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kufanya shambulio la
kudhuru mwili, kuzuia askari kutekeleza majukumu yake na kuzuia ofisa wa umma
kutekeleza majukumu yake.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, Februari 23 mwaka huu nyumbani kwa Zumaridi
katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza kinyume na kifungu namba
241, 243 (b) na 114 (a) na (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Hakimu
Ndyekobora amesema mahakama imewakuta washtakiwa na kesi ya kujibu baada ya
upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa mashahidi 12 na vielelezo 11.
Baada ya
kutamka hivyo akawataka mashahidi kusema watajitetea kwa kiapo au bila kiapo
ambapo wakili wa Utetezi, Steven Kitale amesimama na kuieleza mahakama kuwa
washtakiwa wote watajitetea kwa kiapo.
Baada ya
maelezo hayo, Hakimu, Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo huku akisema ushahidi wa
upande wa utetezi utasikilizwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Oktoba 17 mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment