Mkazi wa Kijijii cha Namanjele mkoani Mtwara,
Somoe Mohamed amemchoma mikono mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano kwa madai
ya kudokoa mboga na kuiba Sh250.
Akizungumza Somoe amekiri kufanya ukatili huo,
akisema lengo lake lilikuwa ni kumwadhibu mtoto kwa tabia mbaya aliyoonyesha"Nilikuwa namwadhibu kwa tabia yake.
Siku ya kwanza alichukua Sh50 na siku ya pili
alichukua Sh200 na baadaye akaanza kudokoa dagaa nikamuonya, lakini hakusikia
mpaka sasa mtoto anasiku tatu tangia amechomwa moto,” amesema.
Baba wa mtoto huyo, Juma Lubega amesema kuwa
yeye alisikia kuwa mwanaye amechomwa moto na mama ake hakuamini lakini
alipofika nyumbani alimuona mtoto akiwa ameungua sehemu ya mikono yake vikiwemo
vidole.
“Nilisikia uchungu kama baba nilipouliza
nikaamibiwa kuwa kaiba Sh250 na kudokoa dagaa, yaani inaonyesha kuwa alimfunga
kamba mikononi akaweka nyasi akamchoma mtoto na inaonyesha alipowasha moto
aliondoka ndio maana mtoto amepata madhara makubwa,” amesema Lubega.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho,
Mussa Mkadimba amesema kuwa tukio hilo sio zuri kwakuwa halifundishi mtoto bali
linaweza kumfanya akawa katili.
“Nimelipokea vibaya hili jambo kwakuwa
halikuletwa kwangu nilisikia niliamua kulifatilia mwenyewe ili kuona kuna
ukweli kiasi gani nikakuta ni kweli mtoto ameunguzwa na moto kwa maeneo ya
mikoa yake.
“Huyu mtoto tangia uchomwe hajapelekwa pelekwa
hosptiali yoyote wala hapata dawa zaidi ya miti shamba wanayotumia kumuwekea
mikononi kutookana na imaini kuwa atapona kwakutumia dawa za asili,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mtwara, ACP Nicodemus Katembo alipoulizwa na mwananchi kuhusu tukio hilo
alisema kuwa yuko safarini na akifika atalifatilia na kulitolea maelezo.
No comments:
Post a Comment