Watu 14 wamefariki
dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota
Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Akizungumza na Mwananchi
kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC),
Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.
Amesema kati ya vifo
hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu
wengine sita walifariki papo hapo
“Ni kweli ajali hiyo
imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari
wanne na dereva na wengine sita waliokuwa kwenye gari lingine” amesema Zakaria
na kuongeza
“Dakika chache
majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki,
wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara” amesema
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Simiyo, Blasius Chatanda amesema yupo katika hospitali ambako majeruhi
walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Robert Gabriel naye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema yuko
njiani kuelekea eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment