Mkuu wa Mkoa wa Tanga ndugu Adam Kigoma Malima ametembelea na Kukagua Ujenzi wa Vituo vitatu vya Afya Wilayani Korogwe ambavyo ni Kituo cha Afya Mgombezi na Kwamsisi vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Kituo cha Afya Mnyuzi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
Akielezea Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Mgombezi
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Ndugu Kalisti Lazaro alisema, "Mheshimiwa Mkuu
wa Mkoa karibu katika Wilaya yetu ya Korogwe, hapa tulipoanzia Ziara yako ni
Kituo cha Afya Mgombezi ambocho kilipokea fedha kiasi cha Tsh 250,000,000/=
tarehe 08/06/2021 na Kituo cha Afya Kwamsisi ambacho kilipokea fedha kiasi cha
Tsh 250,000,000/= tarehe 16/09/2021 na Kituo cha Afya Mnyuzi ambacho kilipokea
fedha kiasi cha Tsh 250,000,000/= tarehe 20/10/2021. Mheshiwa Mkuu wa Mkoa kama
unavyojionea hapa katika Kituo cha Afya Mgombezi Ujenzi upo katika hatua ya
kutandika Jamvi na Kituo cha Afya Kwamsisi kipo kwenye hatua ya kusafisha eneo
na kuweka Michoro kwa ajili ya kuanzia kuchimba Msingi na Kituo cha Afya Mnyuzi
tayari wameshaanza kuchimba Msingi" aliongeza "... Mradi wa Ujenzi wa
Kituo cha Afya Mgombezi unakadiriwa kutumia Jumla ya Tsh 262,831,688 kwa
Majengo yote Mawili, ambapo kiasi cha Tsh 122,789,438 kitatumika kwa Jengo la
Upasuaji na Kiasi cha Tsh 140,042,250/= kwa Jengo la Wazazi na Mpaka sasa kiasi
cha Tsh 11,394,609.75/= zimeshatumika mpaka sasa kwa hatua ya Ujenzi
uliyofikiwa. Makadirio ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kwamsisi kwa Majengo Mawili
ya mwanzo ni Tsh 171,394,791 kwa Jengo la OPD na Tsh 78,352,722 kwa Jengo la
Maabara ambapo kwa sasa tayari Mafundi wameshaanza kuweka alama kwa ajili ya kuchimba
Msingi na Kituo cha Afya Mnyuzi tayari wameshachimba Msingi wa Jengo moja la
Wagonjwa wa nje (OPD)
Hata Hivyo Mh Malima hakufurahishwa na hatua iliyofikiwa
katika Ujenzi wa Kituo cha Afya Mgombezi ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe ndugu
Nicodemus J Bei kuwachukua Wanakamati wa Kituo cha Afya Mgombezi kwenda
Kujifunza kwa wenzao wa Kituo cha Afya Sindeni - Handeni ambao wamefika kwenye
hatua ya Kupaua.
Amesema Vituo
vyote hivyo viliingiziwa hela wakati mmoja na Mkuu wa Mkoa amesema atarudi
baada ya tarehe 01/12/2021 (Wiki mbili na siku mbili) na akute Ujenzi upo
kwenye hatua ya Kupaua na tarehe 01/01/2022 Ujenzi uwe umekamilika na Jengo
likabidhiwe likiwa tayari kwani Mradi huu ni wa siku 90 tuu.
Katika Kituo cha Afya Kwamsisi Mkuu wa Mkoa amemuagiza
Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe baada ya wiki mbili atakuja na akute Msingi
umeshakamilika, na atakuja tena na akute Ujenzi upo kwenye hatua ya Lenta, na
atakuja tena baada ya wiki mbili tena 01/01/2021akute Ujenzi upo kwenye hatua
ya Kupaua na tarehe 15/01/2022 atakuja Kufungua Kituo cha Afya na aliwataka
Wananchi wa Kwamsisi kutoa Ushirikiano katika kulinda Vifaa vya Ujenzi vitakavyoletwa
kwenye eneo la Mradi.
Katika Kituo cha Afya Mnyuzi Mkuu wa Mkoa alifurahishwa na Jitihada za Wananchi na alimuaguza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kuwa Jengo linatakiwa likamilike tarehe 15/01/2021 na alihaidi siku ya Kufungua Jengo atatoa Ng'ombe na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Timotheo Mzava alihaidi kutoa Mchele, huku Diwani wa Kata ya Mnyuzi ndugu Michael Mhina alihaidi kutoa Mbuzi na Mafuta na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe alihaidi kutoa Maji na Soda Kufurahi na Kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea Mradi wa Kituo cha Afya na aliwaonya wale wote wanaozitolea macho Fedha za Miradi ya "Tozo" na "Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano DHIDI ya UVIKO-19" kuwa Fedha za Miradi hiyo si za Kuchezewa na atashughulika na wote watakaobainika kukwapua Fedha hizo.
No comments:
Post a Comment