Aidha baadhi ya watendaji wa madawati hayo wameaswa kuacha masuala ya rushwa ili lutenda haki kwa waathirika wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia haswa watoto
Akizungumza hayo jana Jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa Makamishna na Makamanda wa Polisi Tanzania juu ya upatikanaji wa haki jinai kwa watoto waathirika wa ukatili wa kingono,Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii makao makuu ya Jeshi la Polisi Dk, Mussa Ally Mussa alisema changamoto kubwa inayowakabili wengi katika jeshi hilo kutofahamu kazi na dawati hilo.
Alisema matokeo ya kutofahamu kazi na dawati hilo ni wahusika wakuu wa kusimamia madawati hayo wamejikuta wanawapangia askari wanne hadi sita kwenye madawati badala ya 16 kama muongozo unavyosema.
"Baadhi ya makamanda hamtoi uzito kwenye madawati haya na wengi mnapanga watu wasio na mafunzo ya kushughulikia masuala haya ya udhalilishaji na baadhi yenu mnapanga wagonjwa na wajawazito ambao kimsingi wakiwa hapo hawawezi sababu ya matatizo ya kiafya,maana mjamzito hujikuta mara anashida ya BP au kuvimba miguu hivyo muda wa kusikiliza mtu aliyekumbana na kadhia za udhalilishaji hana, lakini watendaji wenu baadhi wanaua kesi hizi kwa kuendekeza rushwa acheni,".
Aidha alisema kupeleka au kuweka baadhi ya watu waliochanganyikiwa kwenye madawati hayo haisaidii kukabiliana na changamoto za masuala ya udhalilishaji bali inachangia kuongezeka kwa matukio hayo.
Aliwaagiza makamanda hao kuacha pia kupangia kazi za doria watendaji waliopo dawati, kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuacha madawati hayo bila watu kuanzia saa 9:30 jioni na waathirika wa matukio wanapokwenda muda huo kukosa huduma.
"Haiwezekani elimu tunapewa na wadau mbalimbali juu ya madawati haya lakini matukio yanaongezeka hii kwa sababu ya changamoto hizi ebu tujitahidi kuziondoa tutaona mafanikio maana baadhi ya mikoa kesi za matukio ya udhalilishaji na wanawake na watoto yanaongezeka badala ya kupungua,"alisema.
Alisema pia changamoto zinazochangia ongezeko la matukio hayo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kazi ili kuvutia zaidi waathirika kufika katika madawati hayo kutoa taarifa.
Kwamujibu wa Dk.Mussa,askari wa kiume waondokane na dhana madawati hayo ni ya askari wa kike na hata wakati mwingine wakipangwa kukaa kwenye madawati hayo wanakataa kwa madai wao sio wanawake.
"Hili ni kosa na linatokana na sisi wasimamizi wa madawati haya kuwapanga wanawake na matokeo yake watu wamehalalisha kuwa madawati ya wanawake wakati wapo wanaume wanakumbana na matukio ya udhalilishaji na wapofika dawati wakikuta mwanamke wanashindwa kueleza tukio lililomkumba tubadilike tuweke na askari wa kiume,"alisema.
Alisisitiza kila muhusika kusimama katika mafasi yake ili madawati hayo yafanye kazi kusudiwa .
Awali ,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Koshuma Mtengeti alisema kwa kipindi cha miaka mitano matukio ya ukatili wa kingono,ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto yamekuwa yakiongezeka na hadi Julai 12 mwaka huu mikoa inayoongoza katika matukuo hayo ni Arusha (1697),Ilala (1486),Tanga (1347),Kinondoni (924) na Lindi wenye matukio 780.
Pia alisema katika kipindi hicho matukio 6009 ya ukatili wa kijinsia kuwa ya.wripotowa wakati kipindi kama hicho kwa mwaka jana yalikuwa matukuo 7333 hivyo kuna upungufu wa matukio 1324.
Vilevile taarifa ya mwaka 2020 ya takwimu za Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto makao makuu ya polisi imeonyesha kuwepo kwa makosa 42187 ya ukatili wa kijinsia yaliripotiwa vituo vya Polisi Tanzania,ambapo kati yao watu wazima ni 26,333 wanaume 11,102 na wanawake 1,523 na watoto 15,854 kati yao wanaume 3012 na wanawake 1,2842.
Alisema taarifa hiyo inaainisha zaidi kuwa wanawake 1,284 na watoto 5,867 walibakwa ndani ya mwaka 2020na ripoti hiyo inaonyesha watoto 1000 walilawitiwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambao kati yao wanaume 885 na wanawake 115.
Koshuma alisema kama sehemu ya kuimarisha mifumo ya ulinzi na upatikanaji wa haki jinai kwa watoto Tanzania tangu Septemba 2020 CDF imekuwa ikishirikiana na Taasisi ya Irish Rule of law Internatuonal (IRLI) ya nchini Ireland kutekeleza shughuli mbalimbali zenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa haki jinai kwa watoto nchini kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland Tanzania.
No comments:
Post a Comment