OLESABAYA NA WENZAKE SITA WALIVYOCHOTA MILIONI 90 MASHAHIDI 20 NA VIELELEZO 16 KUANZIA TAR 23

 Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusomewa hoja za awali ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa walijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara Fransis Mrosso ili asifunguliwe Kesi ya uhujumu uchumi.

Katika mahakama hiyo leo Alhamisi Septemba 16, 2021, mwendesha mashitaka wa Serikali mkuu, Tumaini Kweka mbele ya hakimu mkazi,  Patricia Kisinda  amesema Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ikiwepo matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa mkuu wa Wilaya ya Hai.

Kweka amesema washtakiwa wengine wote wanakabiliwa na makosa mengine mawili ya kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

Tumaini Kweka akisoma maelezo ya mashtaka hayo amesema makosa hayo yalifanyika Januari 21, 2021 katika eneo la kwa Mrombo jijini Arusha.

Washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Kwema ameeleza mahakama kosa la kwanza linalowakabili washtakiwa wote saba ni kuongoza genge la uhalifu, la pili linalomkabili Sabaya peke yake ni kujihusisha na vitendo vya rushwa na la tatu linalomkabili Sabaya pia ni kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni.

Amedai mahakamani hapo kuwa kosa la nne linalomkabili Sabaya mwenyewe ni matumizi mabaya ya madaraka huku kosa la tano linalowakabili wote saba likiwa ni utakatishahi fedha ambapo wanadaiwa kupata Sh90 milioni huku wakijua kupokea  fedha hizo zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia ameanza kuwasomea maelezo ya makosa hayo.

 

OLESABAYA NA WENZAKE SITA WALIVYOCHOTA MILIONI 90 MASHAHIDI 20 NA VIELELEZO 16 KUANZIA TAR 23 OLESABAYA NA WENZAKE SITA WALIVYOCHOTA MILIONI 90 MASHAHIDI 20 NA VIELELEZO 16 KUANZIA TAR 23 Reviewed by KUSAGANEWS on September 16, 2021 Rating: 5

No comments: