Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirisha kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu mpaka Alhamisi Januari 13, 2022.
Jaji Joachim Tiganga anayeyesikiliza kesi hiyo ameihirisha baada ya shahidi wa nane wa upande mashtaka, Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya (OC-CID) Arumeru, Mrakibu wa Polisi (SP), Jumanne Malangahe kumaliza ushahidi na kuhojiwa na upande wa utetezi.
Upande wa utetezi walianza jana Jumatatu Januari 10, 2022 kumuhoji shahidi huyo
na ukamuomba Jaji kuahirisha kesi hiyo ili kuendelea leo kwa kuwa muda ulikuwa
umeshaenda huku upande huo ukidai kuwa bado ulikuwa na maswali mengi mengi.
Leo asubuhi Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala alianza kumhoji shahidi
huyo mpaka mchana ambapo baada ya kumaliza upande wa mashtaka walimuomba Jaji
aahirishe kesi kwa kuwa hawakumuandaa shahidi mwingine wa kutoa ushahidi kwa
leo.
Baada ya ombi hilo Jaji Tiganga aliwahoji upande wa utetezi ambao uliridhia
ombi hilo na kumfanya Jaji kuahirisha kesi hiyo mpaka Alhamisi ambapo shahidi
mwingine upande wa mashtaka atafika mahakamani hapo kuanza ushahidi.
Sehemu
ya mahojiano kati ya mawakili na shahidi wa nane upande wa mashtaka hii hapa…
Jaji Tiganga ameshaingia na mawakili wa pande zote wanajitambulisha.
Wakili wa utetezi Peter Kibatala anaendelea kumuhoji Shahidi.
Wakili: Katika ushahidi wako kuna mahali Umemzungumzia urio kushiriki katika kutafuta watatu wa kufanya vitendo vya kigaidi
Shahidi: Sijazungumzia.
Wakili: Kwa ufahamu wako uongozi wa Jeshi unafahamu Urio alichokuwa akifanya
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Tunakubaliana vitendo vya kigaidi ni vizito na vinatikisa usalama wa
nchi
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Unafahamu jeshini kuna kitengo kinachochunguza mambo ya kigaidi
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Uliieleza kama mlishirikisha vyombo vingine vya kiusalama ikiwemo TISS
Shahidi: Binafsi sikufanya labda viongozi wenzangu
Wakili: Na katika maelezo yako hakuna mahali uliieleza kama mlishirikisha
vyombo vingine
Shahidi: Sikueleza
Wakili: Unafahamu kama vyombo vingine vingeshirikishwa taasisi kama idara ya uhamiaji
wangeusishwa
Shahidi: Nafahamu
Wakili: Unafahamu shahdi wa nne ndio aliyepanga mpango wote na alidafiri mara
kadhaa kwenda nje ya nchi.
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Unafahamu Rais Samia alipata wapi taarifa hadi kuwatangazia umma kuwa
Mbowe alitoroka nchini
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Ni kweli Mbowe alikimbia nchi kukwepa upelelezi
Shahidi: Sifahamu
Wakaili: Ukiwa kama mpelelezi kuna mtu aliwahi kufungiwa kutokana na tuhuma
hizi za kigaidi
Shahidi: Siwezi kulizungumzia
Wakili: Kwa ufahamu wako kuliwahi kuwekwa zuio la Mbowe kutotoka nje ya nchi
kutokana na tuhuma za kigaidi
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Unafahamu kama miamala za kiuchunguzi ziliwasiliana na nchi ambazo
Mbowe alitembelea
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Agosti 4th 2020 ulijulishwa Mbowe alikuwa akishiriki kula njama za
kutenda ugaidi kwanini kipindi chote Mbowe hakukamatwa
Shahidi: Kulikuwa na mambo mengi ya kiupelelezi
Wakili: Kingine mlichokuwa mnachunguza kwa mwaka mzima
Shahidi: Mambo mengi siwezi kuyazungumzia
Wakili: Mambo gani hayo
Shahidi: Mambo mengi ikiwemo wahalifu wengine
Wakili: Ni watu gani hao na wako wapi hapa mahakamani
Shahidi: Waliachiwa
Wakili: Niambie ni watu gani kama sio kumvizia Mbowe akiwa anaatetea Katiba
mpya
Wakili: Unafahamu nchi nyingi za kidikteta ni kuwakamata wapinzani na kuwapa
kesi za kigaidi
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Unafahamu maana ya trevalla advisor
Shahidi: Sijawahi kukutana na kitu kama hicho
Wakili: Uliwahi kusikia tahadhari yoyote iliyotolewa kwenye mikusanyiko baada
ya 2020
Shahidi: Sijasikia
Wakili: Katika upelelezi wenu Urio ndio alikuwa informer wenu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Na wewe ulikuwa unafanya kazi kufuatana na sheria
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Unafahamu Sheri ya kulinda mtoa taarifa
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Hata hufahamu kwa mujibu wa mtoa taarifa anapokuja kutoa taarifa
mnatakaiwa kumuandikisha maelezo
Shahidi: Sifahamu
Soma hapa:Kesi ya kina Mbowe yaahirishwa, washinda pingamizi
Wakili: Kwa upelelezi wako Mbowe aliwahi kuwapa hawa vijana fedha ya kutoka
Morogoro kwenda Moshi
Shahidi: Kwa maelezo ya Ling'wenya zilipitia kwa Urio
Wakili: Nitafutie sehemu imeandikwa kuwa pesa zilitumwa kwa Urio kwenda kwa
Ling'wenya
Wakili: Wakati fedha zinatumwa Ling'wenya alikuwa anajua rohoni mwake na kwenye
fikra zake alikuwa anaenda kufanya kazi ya VIP protection
Shahidi: Sifahamu kwenye fikra zake
Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ling'wenya alikuwa anajua ni nini anaenda
kufanya nini
Shahidi: VIP protection
Wkili: Nionyeshe ni wapi Urio alimwambia Ling'wenya kuwa anaenda kufanya kazi
ya ugaidi
Shahidi: Hajaonyesha wazi
Wakili: Ni wapi katika maelezo hayo Ling'wenya anakairi alipewa fedha na Mbowe
kwenda kufanya vitendo vya kigaidi
Shahidi: Hakuna
Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji nini kilichowanyima kumpa
vifaa
kama kinasa sauti ili kumsikia Mbowe akipanga vitendo vya kigaidi
Shahidi: Siwezi kulizungumzia hilo
Wakili: Tunakubaliana kuwa hatuna hizo sauti
Shahidi: Kwa nafasi yangu hamna hizo sauti
Wakili: Tuna video au hatuna
Shahidi: Hatuna
Wakili: Mliwahi kumwambia Urio anapoongea na Mbowe aweke kinasa sauti
Shahidi: Sikuwahi kukutana na Urio
Wakili: Mliwahi kuwaza kumpeleka polisi wakati Mbowe anatafuta vijana ajifanye
nni mmojawapo ili a rekodi
Shahidi: Siwezi kueleza
Wakili: Umefahamu lini kama Urio ni mtoa taarifa wenu
Soma hapa:Kina Mbowe washinda pingamizi
Shahidi: Nlifahamu kati ya mwezi wa nane au watisa
Wakili: Ulishiriki kumkamata Tito Magoti
Shahidi: Sikushiriki
Wakili: Unaugomvi na Tito Magot
Shahidi. Hapana
Wakili: Mwambie Mheshimiwa Jaji cheti ulichotakiwa kukileta kama unacho
Shahidi: Nlieleza jana
Wakili: Unacho
Shahidi: Sina
Wakili: Ni wapi Ling'wenya alikiri kushiriki vikao vya kigaidi
Shahidi: Hakuna
Wakili: Nitafutie Mahali Ling'wenya akieleza bastola itakavyotumika kwenye
vitendo vya kigaidi
Shahidi: Hakuna
Wakili: Nionyeshe ni wapi Ling'wenya alieleza vilipuzi vitavyotumika kulipua
vituo vya mafuta
Shahidi: Hakuna
Wakili: Hebu niambie pale Rau madukani uwepo wao ulikuwa unahusiana kupanga
kutekeleza vitendo vya kigaidi?
Shahidi: Walikuwa kwenye mpango huo
Wakili:Unafahamu Adamoo hii bastola na risasi alipata wapi
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Madawa ya kulevya aliyokutwa nayo Ling'wenya mlichinguza amepata wapi
Shahidi: Hatukuchunguza
Wakili: Kwanini hajazungumzia kwenye kesi hii
Shahidi: Hatukuzingumzia
Wakili: Katika uchunguzi wenu mligindua yanahusika vipi na hii kesi
Shahidi: Hatukugundua
Wakili: Nlisika jana ukisema uaskari unashibishwa na kumbukumbu
Shahidi: Kumbukumbu ni moja ya sifa ya askari
Wakili: Ni sahihi Chadema ilijipanga na kushiriki uchaguzi wa mwaka 2020
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Na Mbowe aligombea Ubunge Hai na Tundu Lissu aligombea Urais
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Inakuingia akilini mtu agombee halafu wakati huo akatishe wananchi
wanaoenda kumchagua
Shahidi: Siwezi kuongelea hilo
Kibatala: Unafahamu nyumba na namba aliyokuwa anaishi dada yake Ling'wenya?
Shahidi: Sifahamu.
Wakili: Unafahamu Lujenjwe alikuwa anakaa hoteli gani? Nitajie hata moja.
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Nitajie hata moja.
Shahidi: Alikuwa anakaa hoteli mbalimbali
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mimi nafikiri nimemaliza kumuuliza shahidi maswali.
Kwa Sasa amenyanyuka Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando, kwa ajili ya
kumuuliza maswali shahidi kukusiana na maswali aliyohijiwa na mawakili wa
utetezi kuanzia jana hadi leo
SP Jumanne anafanyiwa cross examination na wakili wa Serikali Mwandamizi,
Robert Kidando
SSA Kidando: Shahidi uliulizwa swali na wakili wa utetezi, kama ACP Kingai kama
alikuwepo Agosti 9, 2020 kituo cha Polisi Mbweni na wewe ukasema hakuwepo
elezea kwanini ulisema hakuwepo?
Shahidi: Tarehe hiyo ACP Kingai hakuwepo kituo cha Polisi Mbeni kwa sababu
alikuwa kwenye kazi ya ufuatilia wengine.
Kidando: Uliulizwa kuhusiana na kukamatwa kwa Gabriel Mhina Agosti 19, 2020 na
kufikishwa mahakamani Sepemba 31, 2020.
Shahidi: Alichelewa kufikishwa Mahakama katika tarehe hiyo kutokana na shughuli
za kipelelezi.
Kidando: Mbowe alikamatwa kwa tuhuma zipi?
Shahidi: Kwa tuhuma za kigaidi na sio za kikatiba.
Kidando: Uliulizwa swali kuhusiana na mshtakiwa wa tatu (Ling'wenya) kufanya
kazi ya VIP Protection na ukasema sio kosa kama mtu atafanya kwa nia njema na
malengo mema, hapa ulikuwa inamanisha Nini?
Shahidi: Nilisema kufanya kazi ya VIP Protection sio kosa, kama mtu atafanya
kwa nia njema lakini kama à tafanya kwa nia ovu hapo ndio kosa.
SSA Kidando: Uliulizwa swali na wakili wa utetezi Dickson Matata kuwa kutumiwa
nauli ni kosa au sio kosa na wewe ukasema sio kosa, kwanini ulisema sio kosa?
Shahidi: Sio kosa kama mtu atatumiwa kwa nia njema.
Kidando: SP Jumanne Uliulizwa siku ulipowakamata mshtakiwa wa pili na watatu
kule Moshi na kuwafikisha kituo Kikuu cha Polisi Moshi na kuhusiana na
kuandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu cha mahabusu( Ditention Register- DR)na
ukasema mshtakiwa hawakuandikishwa katika kitabu hicho, hapo ulimaanisha Nini?
Shahidi: Mtuhumiwa au watuhumiwa wanaandikwa katika kitabu hicho pale tu
anapokuwa ameshikiliwa na kuwekwa mahabusu ndio anaweza kuandikwa kwenye kitabu
hicho (DR)
Kidando: Ulizwa swali katika bastola uliyoikamata kwa mshtakiwa wa Pili,
kulikuwa na maeneo ambayo yangeweza kutoa alama za vidole ukasema ni kweli na
ukasema ushahidi huo wa alama za vidole hukuleta Mahakama, hebu elezea kwanini
ushahidi huo hukuleta Mahakama.
Shahidi: Utambuzi wa alama za vidole sikuleta mahakamani kwa sababu haukuwa na
umuhimu wa kulinganisha nani alikuwa na hiyo silaha kwa sababu ilikamatwa kwa
mshtakiwa huyo na hatukuwa na mashaka na kwamba utambuzi wa alama za vidole(
Fingerprint) hufanyika kama tuna mashaka na mtu ndio huwa tunafanya
ulinganishi.
Kidando: Mheshimiwa Jaji kwa upande wa mashtaka hatuna maswali mengine.
Baada ya wakili Kidando kumaliza Re- examination In chief. shahidi wa nane ( SP
Jumanne) kwa sasa anahojiwa tena na wakili Kibatala.
Jaji: Haya maswali mawili uliyoomba Kitabala.
Kibatala: Naomba nipatiwe kielelezo namba 2 na naomba unisomee.
Shahadi anasoma
Kibataka: Hapo ofisa huyo wa Polisi amesaini maelezo hayo au ameandika namba za
cheo chake?
Shahidi: Amesaini
Kibatala: Huyo ofisa wa Polisi ni rank 5 au laa?
Shahidi: Ni rank 5
Kibatala: Mheshimiwa sina swali
Jaji: Baada ya kumaliza cross examination, upande wa mashtaka mnakitu cha
kumuuliza shahidi?
Kidando: Hatuna cha kumuuliza.
Jaji: Kwa hiyo mmemalizana na shahidi sio?
Kidando: Ndio Mheshimiwa Jaji.
Jaji: Shahidi tunakushukuru kwa uvumilivu wako.
Kidando: Mheshimiwa Jaji, huyo ndio shahidi tuliyokuwa naye kwa leo hivyo
tunaomba ahirisho la kesi hii ili tuje tuweze kuendelea kesho kutwa Alhamisi
tarehe 13 mwezi wa kwanza mwaka 2022 ambapo tutaketa shahidi mwingine kwa ajili
ya kuendelea na shahidi na pamoja ni kwamba saa Saba mchana hatukuweza kuleta
shahidi mwingine kwa sababu hatukujua shahidi huyu angeweza kumaliza saa ngapi.
Hivyo tunaomba ahirishwa kwa sababu kesho ni holiday (Sikukuuu).
Jaji: Upande wa utetezi?
Kibatala: Hatuna pingamizi juu ya alichosema Wakili Kidando.
Jaji: Maombi ya upande wa mashtaka yamekubaliwa, hivyo
Jaji:
Naahirisha kesi hii Hadi siku ya Alhamisi Januari 13, 2022 itakapokuja kwa
ajili ya kuendelea na ushahidi, hivyo naelekeza upande wa mashtaka walete
mashahidi na washtakiwa wataendelea kuwa chini ya usimamizi wa mahabusu.
Mchana mwema.
No comments:
Post a Comment