Miili ya wanahabari na dereva wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza waliofariki katika ajali ya gari jana Januari 11 imewasili katika uwanja wa michezo wa Nyamagana tayari kwa ajili ya heshima za mwisho.
Msafara wa magari
yaliyobeba miili hiyo imewasili uwanjani asubuhi na kuzunguka uwanja kabla
majeneza yaliyobeba miili ya marehemu kushushwa na maaskari wa vikodi vya
ukinzi na usalama na kuwekwa eneo maalum iliyoandaliwa.
Jeneza lenye mwili wa
Ofisa Habari mkoa wa Mwanza, Abel Ngaprmba ndio ulikuwa wa kwanza kushushwa
kwenye gari na kuibua vilio miongoni mwa waombolezaji, hasa waandishi wa habari
na wana familia.
Baada ya jeneza la
Ngapemba, jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Ofisa Habari Halmashauri ya Wikaya ya
Ukerewe Steven Msengi ulishushwa ukifuatiwa na jeneza lenye mwili wa Husna
Mlanzi aliyekuwa mwandishi wa Kituo cha Luninga cha ITV.
Jeneza la nne
kushushwa ni lenye mwili wa Anthony Chuwa aliyekuwa mwandishi wa kujitegemea
akiandikia vyombo mbalimbali vya habari nchini uliofuatiwa na jrneza lenye
mwili wa Jihari Shani wa Uhuru Digital ambaye pia aalikuwa askari polisi.
Jeneza lenye mwili wa
Johari ulibebwa na askari polisi wa kike ikiwa ni sehemu ya taratibu za
kijeshi.
Mwili wa mwisho
kushushwa ulikuwa wa Paulo Silanga aliyekuwa dereva ofisi ya mkuu wa mkoa
aliyekuwa anaendesha gari lililobeba wanahabari siku ya ajali.
No comments:
Post a Comment