Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Taarifa kutoka kwa familia hiyo zinasema kuwa kiongozi huyo
amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa
upasuaji.
Akizungumza Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye
ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa
matatizo ya tumbo.
"Baba alilazwa kama siku tano zilizopita. Wala haina siri,
alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya ikaleta complication
(hitilafu). Alifanyiwa hapo hapo Muhimbili,” amesema Fredrick.
Amesema wanaomba watanzania, kuendelea kumuombea ili afya yake
iendelee kuimarika
"Tunashukuru sana kwa maombi ya Watanzania na tuna imani
ataruhusiwa kurejea nyumbani," amesema.
LOWASA ALAZWA MUHIMBILI TATIZO LA TUMBO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 28, 2022
Rating:
No comments:
Post a Comment