Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wanawake watamuweka madarakani rais mwanamke mwaka 2025.
Samia aliapishwa kuwa
Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John
Magufuli. Kabla ya kupokea kijiti hicho, Samia alikuwa makamu wa Rais wa
Tanzania.
Kwa mujibu wa katiba
ya Tanzania, Rais akifia madarakani, makamu wa Rais huapishwa kuwa
Rais.
“Wameanza kutuchokoza
kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia.
Wanawake bado
hatujaweka Rais mwanamke, rais huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na
matakwa ya katiba, tulichochangia sisi na dada zetu na mama zetu ni ile
kusukuma hadi mwanamke akawa makamu wa Rais ule ndio mchango mkubwa tulioufanya
wanawake, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu
sana, " amesema kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Septemba 15, 2021
alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya demokrasia dunia.
“Sasa ndugu zangu Rais
mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka
rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameaanza kutuchokoza,
kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia."
“Fadhila za Mungu zikija mikononi kwako
usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu ndugu zangu wanawake wamefanya kazi kubwa
kuleta uhuru wa nchi hizi, wanawake tumefanaya kazi kubwa kujenga siasa za nchi
hizi, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hizi leo Mungu ametupa
baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani."
No comments:
Post a Comment