ASKARI wa upelelezi,
Konstable James (31), amedai mahakamani kwamba upelelezi uliofanywa na
kikosi cha makachero, ulibaini kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai
Ole Sabaya na wenzake, walivamia duka la Mohamed Saad, kupiga, kuteka nyara
na kuwaweka chini ya ulinzi watu waliokuwa Dukani hapo |
Hata hivyo, kabla ya
kuanza kutoa ushahidi, washtakiwa walimkataa wakidai kwamba alikuwapo
mahakamani akisikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi wengine lakini
mahakama ilitupilia mbali madai hayo, hivyo kuendelea na ushahidi |
Akiongozwa na Wakili
Mkuu wa Serikali Tumaini Kweka, alidai kwamba ni mpelelezi katika Ofisi ya
Upelelezi Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha (OC-CID) na katika majukumu
yake kituoni hapo amefanya kazi kwa miaka 10 |
James Alidai kwamba
Februari 10, mwaka huu, mlalamikaji Bakari Msangi, alifungua jadala kituoni
kuhusu tukio la shambulio la kudhuru mwili |
Askari huyo alidai
kuwa alikuwa miongoni wa wapelelezi katika shauri hilo na alikabidhiwa jalada
kutoka kwa OC-CID, Gwakisa Minga, Machi 12, mwaka huu, kuanza kupeleleza |
Konstebo James alidai
kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa 11 jioni akiwa ameambatana na OC-CID na
makachero wengine pamoja na Numan Jasin kwenda kufanya upelelezi katika
duka hilo |
Tulipofika katika eneo
hilo, Numan alifungua duka kwa ajili ya sisi kuanza kufanya upelelezi wa
tukio hilo na wakati tukingia dukani tulikuta vitu vikiwa vimesambaratika na
pembeni ya kaunta kulikuwa na majimaji na matone ya damu yaliyoganda |
"Nilimuuliza
Numan kwamba maji yale yalitoka wapi akatueleza kwamba mmoja wa vijana
waliokuwa dukani alijikojolea. Pia wakati tukikagua kutaka kupata uhalisia wa
tukio hilo kwenye CCTV camera, tulibaini kamera nne ‘footage’
zilichezewa," alidai. |
Pia alidai kwamba
wakati wakimhoji Numan, aliwaeleza kwamba Sabaya na walinzi wake
waliwashambulia kwa kuwapiga ngumi, mateke na vibao ndipo walibaini kwamba
kuna kitendo cha kijinai kilifanyika dukani hapo |
"Watu waliopigwa
kwenye tukio ni Hajirini Saada, Numan Jasin na Bakari Msangi na kwa mujibu wa
mhanga (mwathirika) wa tukio hilo, walipigwa na walinzi wa Sabaya
wakishinikizwa kuambiwa sehemu alipokuwa mmiliki wa duka," alidai. |
Pia alidai kwamba
walibaini kamera hizo zilichezewa kwa kugeuzwa kwa kuwa baada ya kuwahoji
wahusika waliwaeleza kwamba kamera hizo hazikuwa katika mwelekeo wake wa siku
zote |
"Katika ukachero
wangu kamera hizo hazikuweza kutusaidia katika upelelezi wetu kwa sababu
zilikuwa zimechezewa, hivyo tukatafuta ushahidi mwingine |
"Katika upelelezi
wangu tulihoji mashuhuda wa tukio hilo na baada ya kuwahoji waliandika
maelezo wakieleza Februari 9, mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni,
walishuhudia magari tatu yakifika katika eneo la duka hilo na walishuka
kwenye watu wapatao 10, akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole
Sabaya, na waliingia ndani na baadhi walibaki nje na mlango wa duka ulifungwa
nusu |
"Mashuhuda hao
walishudia baadhi watu watatu waliokuwa nje walikuwa wameshika
bastola na bunduki kubwa," alidai. |
Kadhalika, alidai
kwamba Bakari Msangi alipokwenda Hospitali ya Mount Meru kutibiwa,
alipigwa picha za mnato mtaalamu wao akiwa na majeraha na walizituma katika
Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (CFB), iliyoko Dar es Salaam kwa ajili ya
upelelezi zaidi |
Alidai kwamba walipiga
picha tano kama sehemu ya kukamilisha ushahidi na kuithibitishia mahakama
kuwa mhanga huyo alipigwa na kushambuliwa |
Shahidi huyo
aliwasilisha mahakamani picha tano za mnato na barua kutoka CFB, ikionyesha
kwamba picha hizo zimefanyiwa kazi katika kamisheni hiyo |
"Baada ya kupokea
majibu hayo nilihakiki picha kama ni zenyewe na niliziambatanisha katika
jalada ya mashtaka," alidai. |
KACHERO ADAI OLESABAYA ALIVAMIA DUKA,AKAIBA NA KUTEKA NYARA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 11, 2021
Rating:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment