Hata hivyo, Mwalimu
mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi
hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni
uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.
"Nilitembelewa na
wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika
shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba
hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza
kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema
Mabula.
Awali, shuleni hapo
yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la
michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na
Tari-Kihinga.
Mmoja wa wazazi hao,
Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya
kupata elimu itokananyo na chanjo.Amesema kitendo cha magari kufika shuleni
hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa
chanjo.
No comments:
Post a Comment