Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Serengeti imemhukumu Juma Makonge (30) mkazi wa Masangura kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia Silaha.
Hukumu ya kesi hiyo ya jinai 21/2020 imesomwa leo Jumanne Machi 30, 2021 na hakimu Judith Semkiwa baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani.
Amesema kwa kosa alilotenda na kifungu alichoshtakiwa nacho adhabu yake inaangukia miaka 30 jela na kuwa milango ya rufaa ipo wazi.
Awali, mwendesha mashtaka wa Serikali, Renatus Zakeo amesema Januari 11, 2020 Juma kwa kushirikiana Chacha Makonge walimvamia Makonge Mwita (90) ambaye ni baba yao na kumkata kwa panga kichwani kisha kumpora Sh3 milioni alizokuwa ameuza ng'ombe mnadani kisha wakakimbia.
Amesema Chacha alikiri kosa na kuhukumiwa miaka 30 lakini Juma akakataa na baada ya ushahidi kuwasilishwa imebainika kuwa alihusika, kuomba mahakama kutoa adhabu kulingana na hitaji la sheria kwa kosa alilotenda.
Mshitakiwa Juma ameomba apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mke na watoto
No comments:
Post a Comment