Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) limemuomba mambo mawili Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo ni kuwa na tume huru ya kweli na maridhiano pamoja na kurejesha mchakato wa kupata katiba mpya.
Bavicha wametoa
mapendekezo hayo leo Jumanne Machi 30,2021 kupitia kwa mwenyekiti wa baraza
hilo, John Pambalu katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema matamshi ya
Samia yanaonyesha ni rais anayependa kufuata utaratibu wa katiba, “sisi Bavicha
tuna mambo mawili makuu tunapenda tuyazungumze ikiwa ni utangulizi wa mwanzo
kuelekea miaka minne iliyosalia kumaliza ngwe hii kuelekea mwaka 2025.”
"Tunaishauri
Serikali umuhimu wa kuwa na tume huru ya kweli na ya maridhiano, tume ambayo
itataka kujiridhisha na kuchunguza kwa kina juu ya uovu wote ambao
umefanyika," amesema.
Pia baraza hilo
limemuomba Rais Samia kuwaachilia huru wafungwa waliofungwa kwa ajili ya
kesi za kisiasa kwa madai kuwa njia hiyo ni nzuri katika jamii.
"Ili kuliponya
Taifa na kuleta maridhiano wapo watu waliokamatwa kwa kesi za kisiasa na
wengine kubambikiwa tunamshauri Rais na Serikali kuelekeza kesi hizo
kufutwa," amesema.
No comments:
Post a Comment