POLISI WELEZA WATU 45 KUFARIKI NA 35 KUJERUHIWA WAKATI WAKIMUAGA RAISI MAGUFULI


Jeshi la Polisi limesema watu 45 walipoteza maisha na 37 kujeruhiwa wakati wa kuuuaga mwili Rais John Magufuli katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli alifariki Machi 17 katika Hospitali ya Mzenana Machi 21 akaagwa na maelfu ya wananchi walifurika Uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho. Wingi wa waomb olezaji hao ulisababisha msururu mpaka nje ya uwanja hivyo kusababisha baadhi yao kukosa hewa kiasi cha kupoteza fahamu.

Mahema yaliyowekwa uwanjani hapo kwa ajili y ahuduma ya kwanza yalijaa hivyo wagonjwa wakalazimika kukimbizwa Hospitali ya Temeke.

Hali ya kujazana uwanjani hapo iliwapa wakati mgumu akina mama hasa waliokuwa na watoto pamoja na wazee ingawa wajumbe wa kamati ya mazishi iliwapa kipaumbele kwa kuwashika mkono na kuwapeleka chumba maalumu kilichowekwa jeneza kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Hali haikuwa mbaya kwa waombelezaji pekee bali vyombo vya ulinzi na usalama pia kwnai vilijikuta katika wakati mgumu wa kuwazuia watu waliokuwa wakilazimisha kuvuka uzio au kuhama sehemu moja kwenda nyingine kutafuta nafasi ya kuuaga mwili huo.

Akizungumza na Mwananchi jana, kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema chanzo cha vifo hivyo ni msongamano wa watu uliosababisha baadhi ya waombolezaji kuruka geti na kulivunja ilmradi wasikose kutoa buriani.

ADVERTISEMENT

“Hawa watu hawakuwa wahalifu, walienda uwanjani kwa ajili ya kumuaga kiongozi wao. Kutokana na wingi wa watu waliokuwa nje, wengine waliruka geti na kusababisha kuvunjika na kuleta maafa hayo,” alisema Mambosasa.

Kamanda Mambosasa alisema majeruhi wote hali zao zinaendelea vizuri na tayari wamesharuhusiwa kuondoka hospitalini ili wakaendelee na majukumu yao. Vilevile aliwaonya wananchi kuwa makini wanapoenda sehemu zenye mikusanyiko mikubwa.

“Kunapokuwa na shughuli yoyote itakayosababisha msongamano, ni vizuri wananchi kufuata utaratibu na maelekezo ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza,” alisema.

Miongoni mwa watu waliofariki uwanjani hapo ni ndugu sita wa familia ya Denis Mtuwa aliyepoteza mke na watoto wawili pamoja na watoto wengine wawili wa shemeji zake. Pamoja nao, alikuwapo Anitha Mfikwa ambaye alikuwa dada wa kazi wa familia hiyo.

Hata hivyo wakati miili ya watoto na mama yao ikizikwa jijini Dar es Salaam, mwili wa Anitha Mfikwa (26) ulisafirishwa kwenda Njombe, nyumbani kwao kwa ajili ya maziko. Katika shughuli hiyo, Mtuwa alimpoteza mkewe, Susan na watoto wawili Nathan na Natalia. Watoto wa shemeji zake Susan walikuwa Christian na Michelle.

Anitha aliambatana na ndugu hao Jumapili ya Machi 21 kwenda kkutoa heshima za mwisho kwa Rais Magufuli lakini wote hawakurudi tena nyumbani wakiwa hai.

Taarifa iliyotolewa Machi 22 na ofisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha ilieleza walipokea majeruhi saba na maiti moja hospitalini hapo kutoka Uwanja wa Uhuru yalikokuwa yakifanyika maombolezo. Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Aza Hamisi, Josseh sunne, Andrew Mirambo na mvulana anaekadiriwa kuwa na miaka 13 ambaye jina halikufahamika. Walikuwapo pia Beatrice Mdake na mwanaume ambaye jina lake halikufahamika.

Katika taarifa hiyo ilielezwa walipokea mwili wa Rose Shabakaki uliohifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini hapo.


POLISI WELEZA WATU 45 KUFARIKI NA 35 KUJERUHIWA WAKATI WAKIMUAGA RAISI MAGUFULI POLISI WELEZA WATU 45 KUFARIKI NA 35 KUJERUHIWA WAKATI WAKIMUAGA RAISI MAGUFULI Reviewed by KUSAGANEWS on March 30, 2021 Rating: 5

No comments: