Faraja Kota, mke wa waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amezungumzia suala la mumewe kuzuia kuingia Kenya akisema mwanasiasa huyo hakuwa na mpango wa kuvuka mpaka kwenda nchini humo bali alikuwa kwenye biashara zake.
Taarifa za kuzuiwa kwa Nyalandu
zilitolewa jana na Novemba 9 na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe
akisema mwanasiasa huyo alikuwa akitaka kuondoka nchini bila kuwa na nyaraka
zinazohitajika.
Alisema maofisa uhamiaji walimzuia
kutoka nchini kutokana na kukosa nyaraka zikiwemo za gari na kumtaka aache gari
hapo mpakani, avifuate vinginevyo watamfikisha mahakamani.
Hata hivyo, akiandika katika ukurasa
wake wa Twitter, Faraja amesema mume wake hakuwa akivuka mpaka kwenda Kenya.
“Hapana, mume wangu hakuwa anajaribu
kuvuka mpaka kwenda Kenya. Hakuhitaji pasi kuwa Namanga kwa ajili ya biashara
zake binafsi upande wa Tanzania mchana kweupe. Tunaishi Arusha. Mungu wangu.
Jambo lenyewe halikutokea jana (Jumatatu) kama ilivyoripotiwa, ni tangu Ijumaa
wiki iliyopita,” ameandika Faraja.
Amewashukuru watu waliojitokeza na
kumjulia hali katika ujumbe huo wakiwemo makada wa vyama vya upinzani.
“Kuna maumivu tunayotakiwa kuponya. Sina nguvu
ya kuwa na hasira. Ninaamini tutapata amani, umoja na huruma kama Taifa. Mungu
aibariki nchi yetu Tanzania.”
No comments:
Post a Comment