Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema kuwa tayari jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Palanga Asia Said, aliyeuawa baada ya kuchomwa mshale usiku wa kuamkia leo wakati akiandaa chakula cha jioni yeye na mume wake.
Kamanda Muroto ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizungumza
na kusema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mume wa marehemu anayejulikana kwa
jina la Hassan Masale, kuwa na ugomvi na mtuhumiwa Haruna Ally, baada ya
kuingiza mifugo kwenye shamba la Alizeti la mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe.
"Tukio limetokea jana majira ya
saa 2 usiku na alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa, na Mshale
uliotumika umekamatwa na mtuhumiwa amekamatwa na amekiri kufanya tukio
hilo", amesema Kamanda Muroto.
Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo kwa lengo la kulipiza kisasi na ndipo alipomvizia mume wa marehemu wakati akiwa nje ili kumchoma mshale na kisha mshale huo kumpata mwanamke badala ya mwanaume.
No comments:
Post a Comment