Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
linamshikilia Flora Adam (23), kwa tuhuma za kumkata mume wake sehemu zake za
siri, ambaye ni Askari polisi aitwaye PC Kazimir (28), mkazi wa Shinyanga
Mjini, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani humo
Deborah Magiligimba, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 28, 2019, majira
ya saa 6:00 usiku, wakati wakiwa wamelala ambapo ghafla mwanamke huyo
alinyanyuka kitandani na kumkata mume wake na kitu chenye ncha kali sehemu zake
za siri.
Baada ya tukio hilo Askari huyo,
alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, ambako
alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa.
Askari Polisi akatwa nyeti zake na mkewe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 02, 2020
Rating:
No comments:
Post a Comment