Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Ulrich Matei amesema kuwa jeneza lililokutwa juu ya meza katika soko la Soweto
mkoani Mbeya, lisihusishwe na imani zozote za kishirikina kwani jeneza lile
lilikuwa ni mali ya msikiti wa Soweto.
Akizungumza leo Januari 2, 2020,
mkoani humo, Kamanda Matei amesema kuwa jeneza hilo lilibebea mwili wa Masoud
Mohamed mkazi wa Makambako, aliyefariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya
Kanda ya Mbeya, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya na ugonjwa wa mapafu.
"Disemba 23, 2019 alifariki na
kuswaliwa katika Msikiti wa Taufiq uliopo Block Q Soweto, mwili wa marehemu
ulihifadhiwa kwenye jeneza kwa ajili ya kusafirishwa Makambako na ulizikwa siku
hiyo hiyo na baada ya kumaliza mazishi jeneza lilibaki kule baada ya kukosa
usafiri wa kulirudisha Mbeya"
amesema Kamanda Matei.
Aidha Kamanda Matei ameongeza kuwa
mnamo Disemba 31, 2019, Ally Mohamed, mkazi wa Makambako alimkabidhi jeneza
dereva wa lori la nyanya ili aweze kulipeleka Mbeya na kumpatia namba ya simu
ya Hamis Mussa Hamad, ili alipokee jeneza hilo.
"Dereva alifika Soweto majira
ya usiku na alivyoipiga simu ya Hamis haikuwa ikipatikana kwa vile alikuwa na
mzigo wa kupeleka Tunduma, ilibidi alikabidhi hilo jeneza kwa mlinzi wa soko la
Soweto ili asubuhi alikabidhi kwa uongozi wa Msikiti huo ambapo naye hakufanya
hivyo" amesema Kamanda Matei.
Polisi yaeleza undani jeneza lililokutwa sokoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 02, 2020
Rating:
No comments:
Post a Comment