Dkt Madeni "Hakuna Mwanafunzi yeyote atakaye kaa Chini mwaka 2020"


Halmashauri ya jiji la Arusha imekabidhi madawati elfu 1000 kwa afisa elimu sekondari wa jiji hilo kwa ajili ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2020.

Akikabithi madawati hayo Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni amesema kuwa kwa jitihada hizo ifikapo januari 6, 2020 hakuna mwanafunzi yoyote wa kidato cha kwanza wala darasa la kwanza atakaye kaa chini.

Dkt Madeni amesama kuwa madawati hayo  yanayotengenezwa na kituo cha ufundi kilichopo chini ya shule ya msingi Kaloleni ni miongoni mwa madawati elfu 3900 yenye thamani ya shilingi milioni 100 ambapo kwa kumia kituo hicho  wameokoa zaidi ya milioni 200 zinazotumika kila mwaka kutengenezea  madawati kwa wakandarasi binafsi.

Amefafanua kuwa kwa takwimu zilizopo kuna upungufu wa madawati 3900 ndani ya jiji la Arusha ambapo baada ya hayo elfu 1000 waliyoyakabiziwa wanatarajia 2900 yaliyobaki hadi kufikia tarehe january 3 yatakuwa yameshakamilika.

Kwa upande wake afisa elimu sekondari wa jiji hilo Mwalimu Valentin Makuka ameeleza kuwa  madawati hayo yatakidhi mahitaji kwa mapokezi ya wanafunzi elfu 1828 wa kidato cha kwanza  ambao wanategemea kuwapokea January 6 ambapo wameongeza jumla ya madarasa 26.
Dkt Madeni "Hakuna Mwanafunzi yeyote atakaye kaa Chini mwaka 2020" Dkt Madeni "Hakuna Mwanafunzi yeyote atakaye kaa Chini mwaka 2020" Reviewed by KUSAGANEWS on December 31, 2019 Rating: 5

No comments: