Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15


Watu 15 wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi nchini Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu, baada ya basi la kampuni ya Harambee kudaiwa kufeli Breki na kuparamia magari mengine saba katikati ya mji wa Moshi.




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.

"Ni kweli kuna ajali imetokea jioni hii eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi  na kwa sasa nipo Mawenzi hospitali, ambapo majeruhi wapo 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine wamepara majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza," amesema Kamanda.

Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.

"Ni mapema sana kuelezea chanzo cha ajali, kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, lakini pia sijapata taarifa ya idadi ya abiria waliokuwepo kwenye basi na magari mengine madogo yaliyohusika katika ajali hiyo" amesema.

Tukio hilo la kuogofya lilinaswa na camera za CCTV, zikionyesha namna basi hilo lilivyoshindwa kuzunguka katika mzunguko huo wa magari na kuparamia magari saba kabla ya kusimama.

Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 Reviewed by KUSAGANEWS on December 17, 2019 Rating: 5

No comments: