Mwanamke
mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa(38) mkazi wa Kijiji cha Mavanga
kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema wilayani Ludewa mkoa wa Njombe
anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo(4)
mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama
Tukio hilo linaleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na kumsukuma mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji
Katika hatua nyingine Olesendeka ameliagiza jeshi la polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.
Katika mahojiano ya awali na jeshi la polisi, mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili amekiri kuua na kukata vipande vipande na kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu akiyatupa porini hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.
Lakini Mume wake bwana Daniel Gumbilo anasema mke wake alisha wahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mototo wao mwingine anaesoma ambapo majirani walinusuru maisha ya mototo wao .
Nae kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa anasema jeshi linaendelea kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.
Kwa upande wa mtendaji wa kijiji cha Mavanga Fadhiri Tajiri alisema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.
"Ni kweli Hilo tukio lipo lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka kwao"alisema Tajiri.
DAR ES SALAAM
Wakati kampeni zikiendelea maeneo
nchini mgombea pekee wa upinzani uenyekiti wa mtaa wa Karikacha manispaa ya
Moshi kwa tiketi ya ACT, Prophil Shayo ameandika barua ya kujitoa baada ya
kufukuzwa uanachama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
(Tamisemi), Mwita Waitara Amesema kuwa katika halmashauri za wilaya 184, kati
ya hizo 90 hazitafanya uchaguzi baada ya wagombea wamepita kupita bila
kupingwa.
Akizungumza Shayo alikiri kupewa
barua ya kufukuzwa uanachama na uongozi wa ACT mkoani humo na Ameleza hayo
akiwa ofisi za msimamizi wa uchaguzi kuwasilisha barua ya kujitoa.
Msimamizi wa uchaguzi manispaa ya
Moshi, Lain Kamendu alithibitisha kupokea barua ya kujitoa mgombea huyo na
kueleza kuwa CCM sasa kimechukua mitaa yote 60.
Naye mweka hazina wa ACT mkoa
Kilimanjaro, Mussa Kamsaa alithibitisha kufukuzwa uanachama kwa Shayo kutokana
na kitendo chake cha kutoandika barua ya kujitoa.
Mwanamke Atuhumiwa Kumchinja Mwanae na Kumla Nyama Ludewa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 20, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment