Rais Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuongoza Watanzania kupokea ndege ya pili aina ya Boeing 787-8
Dreamliner, katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam leo,
shughuli itakayonza saa 8:00 mchana.
Ndege hii mpya imesajiliwa kwa
usajili namba 5H-TCJ na imepewa 'Brand Name' ya RUBONDO ISLAND, visiwa
vilivyopo mkoani Mwanza. Visiwa hivyo vina ukubwa wa kilometa za mraba 456.8,
vikishabihiana na ukubwa wa Manispaa ya Kinondoni iliyopo Dar es Salaam.
Ndege mpya ya Air Tanzania, Boeing
787-8 ina uwezo wa kutembea kilometa 13620 sawa na saa zaidi ya 12 hewani
bila ya kusimama. Inabeba lita 101,000 za mafuta na ina ukubwa wa mita 56.72,
yaani ni sawa na nusu ya Uwanja wa Mpira wa Miguu.
Boeing 787-8 inabeba jumla ya abiria
262, ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 227 yaani 227,930Kg wakati wa kupaa,
uzito huo hujumuisha uzito wa chombo, mizigo na mafuta. Inapotua Inatakiwa iwe
na tani 172 za uzito kutokana na kupungua kwa kiasi cha mafuta.
Sifa nyingine kubwa ya ndege hii ina
uwezo mkubwa wa kuhimili hali nzito ya hewa, ikiwa kwenye umbali mrefu kwenda
juu.
Sifa za ndege mpya inayopokelewa leo na JPM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 26, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment