Watu 10 wamefariki dunia wilayani
Handeni mkoani Tanga baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika
shimo baada ya barabara ya Handeni-Korogwe eneo la Kindeni kusombwa na maji.
Wakati gari hilo likisombwa na maji,
mwingine amefariki dunia katika eneo hilo akiwa katika jitihada za kuvuka eneo
lililojaa maji.
Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26,
2019 mkuu wa Wilaya ya Handeni
Akizungumza baada ya kutembelea eneo
hilo, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema watu 10 wamefariki baada
ya gari kutumbikia katika shimo lililotokana na barabara kusombwa na maji,
mwingine kusombwa na maji.
Tangu jana Ijumaa Oktoba 25, 2019
mamia ya abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani
kuelekea Dar es Salaam na waliotoka Dar es salaam kuelekea mikoa mbalimbali
walikwama katika eneo hilo.
Mbali na watu hao kufariki dunia
baadhi ya kaya zililazimika kuhama makazi yao kwa muda katika Wilaya ya
Korogwe kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Nyumba hizo zilianza kujaa maji
baada ya mto Pangani kufurika na maji kuanza kuelekea katika makazi ya watu.
Mvua yasababisha Vifo vya watu 11 Tanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 26, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment