Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, amewataka vciongozi aliowaapisha leo Ikulu kuwa wavumilivu na
wasihofie kuchafuliwa na watu, bali wajikite zaidi kwenye kutekeleza wajibu wao
kama watumishi wa Umma.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo
Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu
Katibu Mkuu TAMISEMI na Balozi, ambapo kazi ya uongozi inahitaji uvumilivu.
"Kazi za uongozi
zinahitaji uvumilivu, zinahitaji kumtanguliza Mungu mbele, utasemwa,
utachafuliwa lakini ndiyo kazi ya uongozi, naombeni katimizeni wajibu wenu
kaangalieni haki, kaangalieni sheria kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote"
amesema Rais Magufuli
"Kazi hizi ni lazima
tuwatumikie wananchi wanyonge, juzi nilikuwa Mtwara kaimu wa TAKUKURU
anafahamu tulikuta malalamiko kuhusu kulipwa korosho,baada ya kumuagiza
amekuta vyama ushirika 32 vilivyokuwa vinawadhulumu , wananchi wameibiwa Bil.
1. 2" amesema Rais Magufuli
'Ukiwa kiongozi utachafuliwa' - Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 20, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment