Mahakama ya Wilaya ya Musoma mkoani
Mara, imemhukumu Nyamasheki Malima (41), kifungo cha miaka 60 jela, kwa kumkuta
na hatia ya kuwavutisha bangi watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na
13 wa familia moja, kisha kuwalawiti.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa
wiki, Hakimu Jacob Ndira amesema kuwa Malima alitenda makosa hayo kati ya
Septemba 2017 na Septemba 2018, baadaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani na
kusomewa mashtaka yanayomkabili, lakini alikana kufanya kitendo hicho.
Awali, Baba wa watoto hao, ndiye
alikuwa mtu wa kwanza kubaini hali hiyo kwa mtoto mmoja wapo akiwa katika hali
isiyo ya kawaida, baada ya kumfanyia uchunguzi na kuwahoji ndipo walimtaja
mtuhumiwa ambaye alikuwa anawafanyia vitendo hivyo.
Hakimu Ndira, amesema mahakama
ilisikiliza maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kuridhika bila ya kuacha
shaka yeyote huku mshtakiwa akijitetea mwenyewe.
Kwa mujibu wa majibu ya vipimo
yaliyotolewa na daktari aliyewafanyia vipimo watoto hao, unaonesha kuwa sehemu
za haja kubwa zilikuwa zinaingiliwa kila wakati baada ya kuwavutisha bangi
watoto hao ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.
Kutokana na maelezo ya kina ya
kitabibu ya daktari, hakimu Ndira amesema mahakama imejiridhisha watoto
walileweshwa bangi na kulawitiwa.
Hakimu alipo muuliza mshtakiwa kama
ana chochote cha kujitetea kwanini mahakama impunguzie adhabu, yeye alidai hana
nguvu za kiume hivyo asingeweza kufanya kitendo hicho na kuiomba mahakama
imsamehe.
Baada ya utetezi wake Hakimu Ndira
alimwambia mtuhumiwa hana namna ya kupunguziwa adhabu, hivyo atakwenda jela
miaka 60 kutokana na makosa mawili ya kuwavutisha bangi na kulawiti watoto.
Atupwa jela miaka 60 kwa kuvutisha bangi watoto na kuwalawiti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 16, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment