Mkazi wa Kijiji cha Katangara
Wilayani Rombo, Philipina Donath(37) amedaiwa kumuua mtoto wake wa miaka mitano
kwa kumkata na kisu shingoni kisha kujisalimisha mwenye kituo cha polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro Hamis Issah amesema leo Septemba 2019 kuwa tukio hilo lilitokea
jana katika Kijiji cha Katangara Mashati.
"Cha kushangaza mwanamke huyo
baada ya kufanya mauaji ya mwanaye alijisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha
polisi Masharti na polisi walipofika nyumbani kwake walikuta mwili wa mtoto
huyo ukiwa chini huku pembeni mwa mwili huo kukiwa na kisu chenye damu,
"amesema Kamanda Issah.
Pia, amesema polisi wanamshikilia
mwanamke huyo kwa kujihusisha na mauaji hayo.
Amesema mwili wa mtoto huyo
umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma kwa ajili ya taratibu za
mazishi.
Mama aua mtoto wake kwa kumkata kisu shingoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 16, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment