Watano wa familia moja walazwa kwa kula sumu


Watu watano wa família moja wamelazwa hospitali ya wilaya ya Urambo baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu

Akizungumza leo Agosti 24 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kamgembya, kata ya Nsenda wilayani Urambo

Amesema wanafamilia hao watano waliolazwa hospitali ya wilaya wanaendelea vizuri na hakuna yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo
Watano wa familia moja walazwa kwa kula sumu Watano wa familia moja walazwa kwa kula sumu Reviewed by KUSAGANEWS on August 24, 2018 Rating: 5

No comments: