Miili ya watu watatu imetupwa kando kando ya barabara Kijiji
cha Patamela kata ya Saza, wilayani Songwe mkoani hapa, ikiwa na majeraha
kichwani
Mkuu wa wilaya hiyo, Samwel Jeremiah ameagiza kufanyika kwa
uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo na waliohusika. Amesema hata hivyo miili
hiyo bado haijatambulika
“Kweli tukio hilo limetokea na nimeagiza vyombo vyangu vya
ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kuwabaini wahusika na
tunaomba wananchi wawe watulivu kwa kipindi hiki ambacho tunafanya uchunguzi,”
amesema
Shuhuda wa tukio hilo Emmaul Francis, amesema alibaini
miili hiyo leo asubuhi akiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zake
“Nikiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zangu
nimekuta mwili wa mtu ukiwa umelazwa kando ya barabara na baada ya kuona
hivyo nikawataarifu watu walio karibu na eneo hilo na baada ya kuja tukaona
miili mingine miwili ikiwa chini ya karavati ikiwa na majeraha kichwani,”
amesema
Francis amesema baada ya kuona miili hiyo walitoa taarifa
kituo cha polisi Mkwajuni na baadaye miili hiyo ilichukuliwa na kupelekwa
Hospitali ya Mwambani-Songwe
Mganga mkuu wa wilaya ya Songwe, Dk Ibrahim Isack amesema
maiti hizo zote ni za kiume na zimeonekana kuwa na majeraha shingoni na
kichwani
“Sisi watalaamu tunasubiri polisi wafanye uchunguzi wao ili
na sisi tuchunguze kiutalaamu zaidi na baadaye tutaruhusu watu kuja
kuitambua,”amesema Dk Isack
Miili ya watu watatu yatupwa barabarani Songwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 24, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment